Waasi wa zamani wafia kambini Kongo kwa njaa
1 Oktoba 2014Shirika la kimataifa la utetezi wa haki za binaadamu, Human Rights Watch leo limesema hali hiyo inatokana na serikali kushindwa kutoa chakula cha kutosha na huduma za afya kwa waasi hao wa zamani walioamua kuweka silaha zao chini na kujiunga na mchakato wa amani.
Shirika la Human Rights Watch limesema serikali ya Congo inapaswa kuchukua hatua za haraka sana, kuwapeleka wapiganaji hao katika maeneo ambayo wanaweza kupatiwa misaada, kuwafikisha katika mikono ya sheri wale wote waliozembea na kusababisha vifo hivyo na kuuomba Umoja wa Mataifa ushiriki ili kuwarejesha wapiganaji hao wa zamani katika maisha ya kawaida.
Mtafiti mwandamizi wa shirika hilo nchini Congo Idda Swayer amesema serikali ya imewatelekeza wapiganaji hao na familia zao kutokana na kuwachukulia kama waarifu. Alisema kabla ya wote kupoteza maisha serikali inapaswa kwenda mahala walipo haraka na kuwahamishia katika eneo ambalo kunaweza kupatikana chakula, matibabu na mahitaji mengine ya msingi. " Tumegundua zaidi ya wapiganaji 100 wakionyan'nanywa silaha, wake zao na watoto, wamefariki dunia kutokana na njaa na magonjwa katika kambi, baada ya serikali kushindwa kutoa huduma ya chakula la afya".
Septemba 2013, kiasi ya wapigananaji 941 kutoka makundi mbalimbali na mamia ya familia nyingine, walipelekwa katika kambi ya moja iliyopo kaskazini msahariki mwa jimbo la Ikweto iitwayo Katokali. Kwa mujibu wa taratibu zilitoelezwa idadi hiyo ya wapiganaji wa zamani ilikuwa ikisubiri kuingizwa tena rasmi katika jeshi la Congo au waingie katika mfumo wa kiraia.
"Kwa hivyo kwa hivi sasa kumebakia kiasi ya wapiganaji wa zamani 850, na mami ya watu wengine katika filia zao katika kambi hizo". Wapiganaji hao ni kutoka katika makundi ya M23, APCLS, Nyatura na wengine kutoka kundi la Mai Mai.
Serikali imekuwa ikipeleka kiwango kidogo cha chakula na matibabu na kwa kipindi kirefu sana jambo ambalo limesababisha watu hao wafariki dunia kutokana na tatizo la utapiamlo au magonjwa.
Shirika la utetezi la hakin za binaadamu la Human Rights Watch baada ya kufanya uchunguzi katika kambi ya Katokali, mwezi uliyopita lilibaini kutokea kwa vifo vya wanawake watano na watoto 5 katika kambi hiyo tangu Desemba 2013. Katika utafiti wapo huo shirika hilo liliweza kukutana na wapiganaji hao, familia zao na maafisa wa jeshi la Congo ambao wapo katika jukumu la uangalizi wa kambi hiyo.
Wapiganaji hao wa zamani waliliambia shirika la Human Rights Watch kwamba maafisa wa jeshi waliwaambia watazuiwa katika eneo hilo la kambi ya jeshi ya mafunzo ya ukomandoo iliyojengwa 1965, kwa miezi mitatu zaidi. Hata hivyo wanaamini wataweza kujumuishwa jeshini au kuingizwa katika programu ya kuwapaokonya waasi silaha kabla ya kurejea katika maisha yao ya uraia.
Mwandishi: Sudi Mnette/ HRW
Mhariri: Mohammed Khelef