1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi waua 12 Nigeria

1 Januari 2008

---

PORT HARCOURT

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wameshambulia vituo viwili vya polisi,hoteli moja ya kifahari na klabu ya usiku katika mji wa Port Harcout nchini Nigeria na kuua watu 12 leo hii.

Shambulio hilo la mwaka mpya limetokea baada ya wanajeshi kushambulia kwa mabomu maeneo yanayosaidikiwa kuwa maficho ya waasi karibu na mji huo mwishoni mwa wiki pamoja na kuvunjika kwa mazungumzo ya amani kati ya wapiganaji na serikali.

Serikali ya Nigeria haijatoa maelezo juu ya watu waliouwawa kufuatia uvamizi huo lakini vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba watu wengi wameuwawa.Ghasia zimesababisha wafanyikazi wengi wa kigeni wa kampuni za mafuta kukimbia katika eneo la Niger Delta tangu wanamgambo walipoanzisha wimbi jipya la mashambulizi miaka miwili iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW