1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wauwa wakimbizi wengi Uganda.

22 Februari 2004

KAMPALA: Huko Uganda ya Kaskazini waasi wamefanya mauwaji ya halaiki. Kasisi wa Kikatoliki ameripoti kwamba waasi wa lile liitwalo Jeshi la Ukombozi wa Mungu (LRA) wamewauwa watu 170 waliposhambulia kambi la wakimbizi. Wanajeshi wa Uganda wamethibitisha kuuawa wakimbizi 84. Watu wengine 84 walitibiwa hospitalini baada ya kupata majaraha ya kuunguzwa, alisema msemaji wa wanajeshi. Kambi hilo la wakimbizi Barloonyo, liko jimboni Lira, lililoko Kilomita kama 250 Kaskazini mwa mji mkuu Kampala. Jeshi hilo la Ukombozi wa Mungu linawatumia watoto waliotekwa nyara kama wanajeshi wake na kuwashirikisha kwa nguvu katika harakati za mauwaji. Kundi hilo la waasi linapigana tangu miaka 17 kuungusha utawala wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW