1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Waasi wachukua udhibiti wa mji wa Tidermene, Mali

13 Aprili 2023

Wapiganaji wenye itikadi kali na wenye mafungamano na Kundi la Dola la Kiislam, wamechukua udhibiti wa mji wa Tidermene nchini Mali baada ya kushuhudia mapigano makali kwa miezi kadhaa.

Symbolbild Islamisten in Burkina Faso
Picha: ROMARIC OLLO HIEN/AFP/Getty Images

Afisa mmoja wa serikali aliyekimbia mji huo amelithibitishia shirika la habari AFP kwamba, mji huo upo chini ya udhibiti wa kundi  la wapiganaji wa Daesh, huku wakiwataka wakaazi kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kulipa ushuru kwa kundi hilo.

Kuendelea kushamiri kwa harakati za uasi nchini Mali  kumesababisha mamia ya raia kuuwawa, huku wengine mamilioni wakivuka mpaka na kuingia taifa jirani la Niger.

Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu yanasema 'Wanajihadi' wamefanya mashambulizi ya adhabu dhidi ya jamii wanazozituhumu kusaidia serikali au kukataa kujiunga na harakati zao.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW