1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waathiriwa wa Ukimwi bado wakumbwa na umaskini

Admin.WagnerD1 Desemba 2011

Hii leo dunia nzima inaungana pamoja katika kuadhimisha siku ya ukimwi dunian huku maelfu ya watu wanaougua ugonjwa huo nchini Asia wakikumbwa na umaskini kutokana na maisha magumu ya kuishi na ugonjwa huo.

ILLUSTRATION - Eine rote Aids-Schleife liegt auf einem Globus über dem Kontinent Afrika, aufgenommen in Frankfurt (Oder) am 29.11.2010. Die WHO hat den 1. Dezember als den Weltaidstag 1988 ausgerufen. Rund um den Globus erinnern am 1. Dezember verschiedenste Organisationen an das Thema Aids und rufen dazu auf, aktiv zu werden und Solidarität mit HIV-Infizierten, Aids-Kranken und den ihnen nahestehenden Menschen zu zeigen. Foto: Patrick Pleul dpa/lbn
Nembo ya mapambano ya Ukimwi na VVU.Picha: picture-alliance/dpa

Kulingana na shirika la umoja wa mataifa huku wanawake na watoto ndio walikumbwa zaidi na hali hiyo ya kuishi na virusi ya ukimwi. kodi ya juu ya huduma ya afya, kukosa ajira kutokana na mtu kuambukiwa virusi, na unyanyapaa mkubwa dhidi ya watu wanaoishi na virusi hivyo huwaweka katika nafasi ngumu ya maisha.

Naibu mkurugenzi wa mipango ya maendeleo wa umoja wa mataifa Nicolas Rosellini amezitaka serikali za maeneo ya Asia zijitahidi katika kuinua maisha ya wanaoishi na virusi vya ukimwi. Rosellini amesema matumizi ya ziada ya fedha kwa watu hao inawapa changamoto katika kuwalipia watoto wao karo za shule, amesema hii inasababisha idadi ya watoto wanaowacha shule kuzini katika maeneo hayo.

Ripoti hii ya umoja wa mataifa pia imesema wanawake na watoto ndio walio hatarini zaidi ya kuambukizwa virusi, hawapati huduma nzuri ya afya na wao ndio wanaotekwa jukumu la kuwaangalia wale wanaooua ugonjwa huo. Nchi kama India Indonesia na Vietnam wanaougua virusi vya ukimwi huko wanatumia fedha nyingi zaidi ikiwa mara mbili au tatu ya mtu ambaye hana virusi.

Umoja wa Mataifa unakadiria watu millioni 34 ulimwengiuuni wanaishi na virusi vya ukimwi huku vifo vinavyohusiana na ugonjwa huo vikipungua kutoka milioni 2.2 hadi milioni 1.8 mwaka uliopita.

Mtaalam wa magonjwa ya UKIMWI na VVU Dr. Melanie Francoise Nzouaton wa CameroonPicha: DW

Sababu kuu ambazo zinahusishwa na maambukizi ya haraka ya ukimwi ni kufanya ngono isio salama, utumiaji wa madawa ya kulevya hasa matumizi ya kutumia sindano za pamoja, ukahaba na ushoga ambao unachangia asilia 15 ya maambukizi.

Tukutupia macho Afrika mashariki, sasa kenya inaidhini ya kutengeneza dawa za kupunguza makali za ukimwi maarufu kama arvs. Shirika la afya duniani WHO ilitoa idhini hiyo kwa kampuni moja nchini kenya November 16 mwaka huu. Kenya sasa imechukua nafasi ya nne afrika mashariki kuwa miongoni mwa mataifa yalioidhinishwa kutengeneza madawa haya.

Kwa sasa hivi Afrika mashariki inakumbwa na uhaba wa madawa haya ya ARVs. Nchini Kenya thuluthi tatu ya watu laki 8 wanauwezo wa kupata dawa hizo.

Professa Alloya Orago mkurugenzi mkuu wa baraza la ksuhughulikia maswala ya ukimwi Kenya, amesema kwa sasa kenya itakuwa na nafasi ya kutengeneza madawa haya na hata kuyauza katika mataifa jirani ya Afrika mashariki na kuboresha kwa kiwango kikubwa uwezo wa kuishi zaidi kwawagonjwa wa ukimwi .

Kauli mbiu mwaka huu katika kuadhimisha ukimwi ni kuangamiza kabisa ugonjwa wa ukimwi, kukomesha unyanyapaa na ubaguzi pamoja na kupunga vifo.

Mwandishi: Amina Abubakar/AFPE
Mhariri: Mohammed Abdulrahman