Wabadilisha pasipoti wanasubiri muda mrefu Ujerumani
4 Agosti 2024Matangazo
Maombi yanaelezwa kuongezeka baada ya mabadiliko ya taratibu za utoaji wa pasipoti hizo kuanza kutumika rasmi Juni 27, yakilenga kupunguza masharti ya mtu kustahili kupata uraia wa nchi mbili.
Mkuu wa ofisi ya chama kinachowakilisha maslahi ya miji ya Ujerumani, Helmut Dedy aliliambia shirika la habari la DPA kwamba dhamira ilikuwa sio tu kuurahisishia umma kuipata pasipoti hiyo lakini pia kwa uharaka zaidi.
Sheria mpya ya uraia, iliyopitishwa na muungano wa mrengo wa kati wa Kansela Olaf Scholz, kadhalika inatoa fursa ya watu kutuma maombi ya uraia baada ya kuishi Ujerumani kwa miaka mitano, badala ya mahitaji ya hapo awali ya miaka minane, ili mradi watimize masharti yote.