1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabakaji Bint wa Yombo wafungwa maisha, faini milioni moja

Deo Kaji Makomba
30 Septemba 2024

Watu wanne walioshitakiwa kwa kosa la kumbaka na kumuuingilia kinyume cha maumbile binti mmoja wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kifungo cha maisha jela na faini ya shilingi milioni moja kwa kila mmoja.

Tanzania I Dodoma
Gari la Magereza mbele ya mahakama ya hakimu mkaazi, Dodoma, Tanzania.Picha: Deo Kaji Makomba/DW

Katika kesi hiyo ya jinai Namba 23476 ya mwaka 2024, MT 140105 Clinton Damas maarufu kama Nyundo, ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari magereza C. 1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson na Amin Lema, wamekutwa na hatiya ya kumbaka na kumuingilia kinyume cha maumbile binti mmoja wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam na hivyo kuhukumiwa kifungo cha maisha jela na faini ya shilingi milioni moja kila mmoja.

Soma zaidi: Viongozi wakuu wa Chadema nchini Tanzania waachiliwa kwa dhamana

Akizungumza mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo katika kesi iliyosikilizwa faragha kwenye Mahakama ya Hakimu Mkaazi Dodoma, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mashitaka ya Taifa, Lenatus Mkude, alisema serikali imeridhishwa na hukumu hiyo.

Kwa upande wake, wakili wa utetezi wa washitakiwa, Godfrey Wasonga, alisema kuwa pamoja na kuheshimu maamuzi ya mahakama, lakini wataukatia rufaa uamuzi huo.

Kesi hiyo ilivuta hisia za watu wengi hasa kutokana vidio iliyosambaa mtandaoni ikiwaonesha waliokuwa wakituhumiwa kufanya tendo hilo wakiwa hawana wasiwasi wowote.

Tukio hilo lilizua hasira kubwa kwa wananchi wakitaka hatua kali za kisheria zichukuliwe.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW