JamiiAsia
Wabengali waandamana dhidi ya waliobadilisha jinsia
26 Januari 2024Matangazo
Afisa wa polisi katika mji mkuu, Dhaka, Zakir Hossain amesema takriban watu 5,000 walijiunga kwenye maandamano hayo yaliyofanyika nje ya msikiti katikati mwa mji huo.
Maandamano hayo yaliandaliwa na moja ya vyama vikubwa vya Kiislamu nchini Bangladesh.
Soma zaidi: Maelfu waandamana Bangladesh kumtaka Waziri Mkuu kujiuzulu
Waandamanaji hao waliimba nyimbo za kuwataka watu wanaohusika na mapenzi ya jinsia moja kuondoka katika nchi hiyo yenye Waislamu wengi.
Wanawake waliobadili jinsia zao wanatambuliwa kisheria nchini Bangladesh kama watu wa jinsia ya tatu.
Marekebisho ya mtaala mwaka uliopita yalijumuisha kutambuliwa wanawake hao katika vitabu vya shule.