1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Wabunge Japan wampigia kura Ishiba kuendelea na uwaziri mkuu

11 Novemba 2024

Wabunge nchini Japan, wamempigia kura Shigeru Ishiba kuendelea na wadhifa wa waziri mkuu, licha ya kuuongoza muungano wake tawala katika matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi mkuu ndani ya miaka 15.

Bunge la Japan
Wabunge wamemteua Ishiba kuwa waziri mkuu wa serikali ya wachache, hatua inayomuweka katika hali ya msukosukoPicha: Eugene Hoshiko/AP Photo/picture alliance

Wabunge wamemteua Ishiba kuwa waziri mkuu wa serikali ya wachache, hatua inayomuweka katika hali ya msukosuko wa kisiasa au kuhitaji maelewano zaidi ili kupitisha miswada mipya.

Soma pia: Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba aahidi kufanya "mageuzi ya msingi"

Ishiba, aliye na umri wa miaka 67 na waziri wa zamani wa ulinzi, aliingia madarakani wiki sita zilizopita na kufanya uchaguzi wa mapema mnamo Oktoba 27.

Soma pia: Muungano tawala Japan wapoteza wingi wa viti bungeni

Alikuwa na matumaini ya uungwaji mkono mkubwa kama kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Liberal Democratic, LDP. Ishiba aliingia madarakani kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Fumio Kishida, aliyeng'atuka kufuatia kashfa ya ufisadi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW