Wabunge nchini Kenya wataka watambuliwe kuwa kundi rasmi la upinzani.
22 Aprili 2008Matangazo
Hoja wanayotoa ni kwamba ni takwa la wananchi wa Kenya kuwa na upinzani rasmi bugneni na ni haki kwa serikali kusailiwa na kuchunguzwa nini inafanya; hiyo ni nguzo muhimu ya mfumo wa demokrasia. mmoja wa wabunge waliotia saini kuunga mkono dai hilo ni yule wa Budalanyi, magharibi ya Kenya, Bwana Ababu Namwamba.
Othman Miraji alizungumza naye na alimwambia umbali gani hatua yao imefikia.