Wabunge, Tanzania waipa serikali madaraka makubwa
30 Januari 2019Bunge la Tanzania limepitisha mswada wa mabadiliko jana jioni ambao unatoa madaraka makubwa kwa msajili wa vyama vya siasa ambaye anateuliwa na serikali, hatua ambayo wabunge wa upinzani wanasema itaimarisha utawala wa chama kimoja.
Serikali ya Rais John Pombe Magufuli tayari imekwisha piga marufuku baadhi ya magazeti, kuzuwia mikutano ya vyama vya upinzani na kuwakamata wanachama kadhaa wa vyama hivyo, pamoja na kuingilia kati mara kwa mara kwa serikali katika sekta muhimu kama madini na kilimo, na kudhoofisha uwekezaji katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa wa tatu katika eneo hilo.
Mabadiliko hayo yanampa msajili anayeongozwa na serikali madaraka makubwa kuweza kukifuta chama na kutoa hukumu ya hadi mwaka mmoja jela kwa mtu yeyote anayefanya harakati za elimu ya raia ambayo haikuidhinishwa, kwa mfano utaratibu wa kujiandikisha kupiga kura.
Viongozi wa upinzani wanasema mabadiliko hayo ya sheria yatanya shughuli za kisiasa kuwa uhalifu na kuigeuza Tanzania kuwa ya chama kimoja.