1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge Thuringia wamchagua spika kutoka CDU

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Bunge katika jimbo la mashariki mwa Ujerumani la Thuringia, limemchagua Thadeus Koenig wa chama cha kihafidhina cha Christian Democratic Union, CDU, kuwa spika wake mpya jana Jumamosi.

Thüringia | Spika mpya wa Bunge Thadäus König-CDU
hadäus König (CDU) Spika mpya wa Thüringia.Picha: Martin Schutt/dpa/picture alliance

Koenig alikuwa anashindana na mteule wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, Wiebke Muhsal. Alipata wingi wa kura 54 kati ya jumla ya kura 88 kwa kuungwa mkono na vyama vya mrengo wa kati na vile vya mrengo mkali ya kushoto.

Hayo yametokea licha ya chama cha AfD kuibuka cha kwanza katika uchaguzi wa Septemba 1 jimboni Thuringia, kwa kupata asilimia karibu 33 ya kura. Chama cha CDU kilishika nafasi ya pili kwa kupata karibu asilimia 24 ya kura.

Soma pia:Kiongozi wa chama cha CDU Friedrich Merz kugombea ukansela

CDU kinajaribu kuunda serikali jimboni Thuringia kwa kuiweka kando AfD. Ili kuunda serikali ya muungano jimboni humo, CDU inafanya majadiliano na chama cha mrengo wa kati-kushoto cha SPD, na kile kipya cha mrengo mkali wa kushoto cha Muungano wa Sahra Wagenknecht, BSW.