1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge Ujerumani: Mjadala wa kuwarejesha Wasyria ufanyike

18 Desemba 2024

Wabunge waandamizi wa kihafidhina katika bunge la Ujerumani, Bundestag, wamewataka wanadiplomasia Damascus kuzungumzia uwezekano wa kuwarudisha Syria, wakimbizi, katika mazungumzo na viongozi wa utawala mpya wa Syria.

Mkuu wa chama cha upinzani Ujerumani cha Christian Social Union CDU Alexander Dobrindt
Mkuu wa chama cha upinzani Ujerumani cha Christian Social Union CDU Alexander DobrindtPicha: Kay Nietfeld/picture alliance/dpa

"Ni muhimu kwa suala la uhamiaji na kurudishwa makwao yakahusishwa na uwezekano wa misaada ya ujenzi mpya wa Syria," alisema kiongozi wa chama cha Christian Social Union CSU, Alexander Dobrindt.

Chama cha CSU na chama chake ndugu cha Christian Democratic Union CDU,ndio muungano mkubwa wa upinzani katika bunge la Ujerumani na wanaongoza katika tafiti za maoni kuelekea uchaguzi wa mapema utakaofanyika Ujerumani Februari 23, mwaka 2024.

Karibu Wasyria milioni 1 wanaishi Ujerumani kwa sasa, wengi wao wakiwa walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha umwagikaji wa damu kwa zaidi ya mwongo mmoja na pia ukatili wa rais wa zamani Bashar al-Assad.

Al-Assad aliikimbia Syria mapema mwezi huu baada ya muungano wa makundi yaliyojihami yaliyokuwa yanaipinga serikali yake, wakiongozwa na wanamgambo wa Kiislamu wenye misimamo mikali, kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kuiteka miji miwili mikubwa nchini humo Aleppo na Damascus.

Kundi la Hayat Tahrir al-Sham HTS, ambalo linatambuliwa kama kundi la kigaidi na Umoja wa Ulaya na wengine, ndilo linaloongoza harakati za kuunda serikali ya mpito Damascus.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW