1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Marekani kujaribu tena kuchagua Spika

4 Januari 2023

Wabunge wa Republican nchini Marekani, watajaribu tena leo kuukwamua mkwamo wa kumpata spika mpya baada ya duru tatu za upigaji kura.

Kongressausschuss stimmt für Veröffentlichung von Trumps Steuererklärungen
Picha: Andrew Harnik/AP/picture alliance

Kiongozi wa chama cha Republican, Kevin McCarthy, alishindwa kupata kura za kutosha ili kuchaguliwa spika wa Baraza la Wawakilishi.

Mwanasiasa huyo kutoka California alihitaji kura 218 kati ya 434. Hii ni mara ya kwanza katika karne moja, kwa Warepublican kushindwa kumchagua spika hata baada ya majaribio matatu.

McCathy amesema atasalia kwenye kinyang'anyiro hicho cha uspika.

Rais wa zamani, Donald Trump, ametoa wito kwa wajumbe wa Republican kumuunga mkono McCarthy.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW