1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wabunge wa Marekani wakutana na Dalai Lama

19 Juni 2024

Kundi la wabunge wa Marekani, akiwemo spika wa zamani Nancy Pelosi, limekutana na kiongozi wa kidini wa Tibet, Dalai Lama, na serikali ya Tibet iliyo uhamishoni nchini India, hatua iliyokosolewa vikali na China.

India, Marekani, Dalai Lama
Ujumbe wa wabunge wa Marekani wakiwa na kiongozi wa kidini wa Tibet, Dalai Lama, anayeishi uhamishoni kaskazini mwa India.Picha: REUTERS

Wabunge wanaoongozwa na mbunge Michael McCaul na Pelosi walimtembelea kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88 nyumbani kwake katika mji wa milimani wa Dharamsala ulioko kaskazini mwa India.

Ziara hiyo inafuatia hatua ya bunge la Marekani kupitisha muswada unaoitaka China ifanye mazungumzo na viongozi wa Tibet.

Soma zaidi: Spika wa bunge la Marekani akutana na Dalai Lama

Ubalozi wa China nchini India umeilaani ziara hiyo ukisema Dalai Lama si kiongozi wa kidini, bali ni mwanasiasa aliye uhamishoni anayehusika na vitendo vya kuipinga China huku akijificha kwenye dini.

Raia wengi wa Tibet walio uhamishoni wanahofia kwamba Beijing itamteuwa mrithi wa Dalai Lama na kuongeza udhibiti wake Tibet.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW