Wabunge wa Marekani wavutana kuhusu matumizi ya serikali
15 Julai 2011Matangazo
Geithner amewaambia wabunge wa vyama vya Demokratik na Republikan kuwa ulimwengu unapaswa kupewa ishara moja kwa moja, kuwa Marekani inaweza kutekeleza wajibu wake wa kulipa madeni.
Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani, Ben Bernanke pia, ameonya kuwa hatua ya kupunguza matumizi ya serikali kwa kiwango kikubwa, huenda ikazuia ukuaji wa kiuchumi ulio dhaifu na hivyo kuathiri uchumi wa Marekani na ulimwengu mzima.
Shirika la Moody's linalotathmini uwezo wa taifa kulipa mikopo, limeonya kuishusha Marekani katika tabaka la chini kwa sababu ya majadiliano ya bajeti kutosonga mbele. Hata shirika la China, Dagong limeeleza fikra kama hiyo.