1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNamibia

Namibia yapitisha sheria dhidi ya ndoa za jinsia moja

20 Julai 2023

Wabunge nchini Namibia wameidhinisha sheria ya kupiga marufuku ndoa za jinsia moja na kuwaadhibu wale wote watakaokiuka sheria hiyo. Sheria hii ambayo haikupata upinzani wowote bungeni.

Made Sendung für den 11.07.2023
Picha: DW

Wabunge nchini Namibia wameidhinisha sheria ya kupiga marufuku ndoa za jinsia moja na kuwaadhibu wale wote watakaokiuka sheria hiyo. Sheria hii ambayo haikupata upinzani wowote bungeni, inalenga kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Juu ulioruhusu kutambuliwa kwa baadhi ya ndoa za mashoga zilizofungwa nje ya nchi.

Mbunge wa Chama tawala cha SWAPO, Elder Philipe, amesema suala la muungano wa familia ni kati ya mwanamme na mwanamke na hilo linapaswa kuheshimiwa, akisisitiza kuwa kufanya tofauti na hivyo ni kwenda kinyume na maadili.

Soma Zaidi: Museveni asaini sheria ya mapenzi ya jinsia moja

Wakosoaji wamesema huu ni ukandamizaji ambapo mwanaharakati na mtetezi wa haki za mapenzi ya jinsia moja, Zindri Swartz, amesema kuwa sheria hiyo ni mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya jamii ya watu hao na ukiukwaji mkubwa wa utu na ubinaadamu.

Mapenzi ya jinsia moja yamepigwa marufuku nchini Namibia chini ya sheria ya ulawiti ya mwaka 1927 ambayo, hata hivyo, imetumika mara chache mno.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW