1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Wabunge wa Republican waukosoa mpango wa amani wa Trump

27 Novemba 2025

Wabunge kadhaa wa chama cha Republican nchini Marekani, wameukosoa vikali mpango wa amani uliopendekezwa na Rais Donald Trump ili kumaliza vita vya Ukraine, wakisema mpango huo unaipendelea Urusi.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa kwenye ndege ya Air Force OnePicha: Alex Brandon/AP Photo/dpa/picture alliance

Washirika wa Ukraine wana wasiwasi kwamba utawala wa Trump unaweza kuishinikiza Kyiv kusaini mpango huo wenye vipengee 28  uliotangazwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.

Mpango huo unaitaka Ukraine kuachia baadhi ya maeneo kwa Urusi, kupunguza idadi ya jeshi lake na kuahidi kutojiunga na Jumuiya ya kujihami ya NATO.

Wakati huohuo, Marekani inaendelea na juhudi za kufanikisha mpango huo wa amani. Katibu Mkuu wa Jeshi la Marekani Daniel Driscoll sasa anafanya mazungumzo na ujumbe wa Urusi huko Abu Dhabi, baada ya kukutana na maafisa wa Ukraine mjini Kyiv.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW