JamiiUganda
Bunge la Uganda kuupigia kura muswada wa kupinga ushoga
21 Machi 2023Matangazo
Sheria hiyo inapendekeza hatua mpya kali zichukuliwe kwa watu wanaojihusisha na mahusiano ya aina hiyo nchini Uganda ambako ushoga ni kitendo kisichokubalika.
Chini ya sheria inayopendekezwa, mtu yoyote anayehusika na vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja au yeyote atakayejitambulisha hadharani kama mwanachama wa kundi la LGBTQ anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela.
Soma pia: Uganda yapanga kutunga sheria mpya ya kupinga ushoga
Mwenyekiti wa kamati inayoshughulikia masuala ya bunge na ya kisheria Robina Rwakoojo amesema muswaada huo uko tayari na utapigiwa kura leo mchana baada ya kusikilizwa hoja za pande zote mbili ule wa wanaounga mkono na wale wanaoupinga muswaada huo na mapendekezo yaliyotolewa kuzingatiwa.