Wabunge wa Uhispania waanza kujadili muswaada wa msamaha
13 Desemba 2023Kutolewa kwa msamaha kwa wanasiasa wa jimbo hilo tajiri ilikuwa sehemu ya ahadi za Waziri Mkuu Pedro Sanchez kusalia madarakani.
Mjadala huo ulioanza jioni ya jana, unafanyika ikiwa ni miaka sita tangu jaribio lililoshindwa la kutangaza uhuru wa Katalunya, huku Sanchez akisema msamaha huo utasaidia kufunguwa ukurasa mpya.
Soma zaidi: Uhispania baada ya Uchaguzi wa Bunge
Wabunge 178 kati ya 350 waliridhia kuanza kujadiliwa kwa msamaha huo. Wabunge hao pia waliridhia kuanzishwa kwa kamisheni tatu zinazotakiwa na vyama vinavyopigania kujitenga kwa Katalunya, ili kuiunga mkono serikali ya mseto ya Sanchez.
Mojawapo ya kamisheni hizo ni ile ya kuchunguza kashfa ya ujasusi dhidi ya viongozi wa Katalunya kupitia programu ya Pegasus baada ya kushindwa kwa jaribio la uhuru mwaka 2017.