1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza kuijadili sheria ya kuwapeleka wakimbizi Rwanda

16 Januari 2024

Wabunge wa Uingereza wataujadili tena mpango tata wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda. Mpango huo ni mtihani kwa Waziri Mkuu Rishi Sunak, wakati uchaguzi mkuu ukiwa unakaribia nchini humo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akilihutubia bunge la UingerezaPicha: ROGER HARRIS/UK PARLIAMENT/AFP

Rishi Sunak aliye madarakani tangu Oktoba mwaka 2022 ameiweka hatma yake ya kisiasa katika kupunguza viwango vya uhamiaji halali na haramu na hivyo mswada wa serikali yake unaoinadi Rwanda kuwa ni sehemu salama ya kuwapeleka wakimbizi uliopewa jina la (Ukimbizi na Uhamiaji) ni muhimu kwa kuitimiza ahadi hiyo ya Waziri mkuu wa Uingereza.


Mswada huo tata, hata hivyo, umesababisha mivutano ndani ya chama tawala cha Consevartives. 


Mwezi uliopita Sunak alishinda kura bungeni kuhusu sheria hiyo na sasa ni lazima ashinde kwa mara nyingine tena, katika kura inayotarajiwa kufanyika hapo kesho Jumatano usiku.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW