Mishahara ya wabunge
21 Mei 2008
Wabunge wa Ujerumani wamekataa pendekezo ambalo lingewezesha mishahara yao kuongezwa kwa asilimia 16 nukta 4 .
Pendekezo hilo pia lilipingwa vikali na vyama vya upinzani pamoja na wananchi.
Pendekezo la kuongeza mishahara ya wabunge 612 hapo awali pia liliungwa mkono na kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliesema kuwa lengo lilikuwa kusawazisha mishahara ya wabunge na ya mahakimu.
Lakini ,kwa mujibu wa vyombo vya habari kansela Merkel na baraza lake la mawaziri pia wapo tayari kusamehe nyongeza za mishahara yao.
Msemaji wa serikali ya Ujerumani ameeleza kuwa Kansela Merkel alitangaza uamuzi huo mapema leo kwenye baraza lake la mawaziri.
Kutokana na malalamiko makubwa ya wananchi viongozi wa vyama vya CDU na SDP vinavyoongoza serikali ya Ujerumani waliamua jana kusimamisha mpango juu ya kuongeza mishahara ya wabunge wa vyama vyao.
Mishahara hiyo ingelifikia Euro 7,946 kwa mwezi.