Korea Kusini kupiga kura ya kumfungulia mashtaka rais
5 Desemba 2024Hayo yanajiri wakati waziri wa ulinzi anayeshtumiwa kwa kumshauri rais huyo juu ya kutangaza sheria ya kijeshi akijiuzulu.
Wabunge hao kutoka chama cha upinzani cha Democratic wamepanga kupiga kura bungeni ya kumfungulia mashtaka Yoon siku ya Jumamosi. Haya ni kulingana na msemaji wa chama hicho aliyewaarifu waandishi wa habari.
Awali, mbunge wa chama hicho cha Democratic, Kim Seung-won, aliliambia bunge kwamba tangazo la serikali ya Yoon ya sheria ya dharura ya kijeshi lilisababisha kuchanganyikiwa na hofu kubwa miongoni mwa raia wa nchi hiyo.
Soma pia: Chama tawala Korea Kaskazini chagawika kuhusu rais
Chama tawala cha Yoon cha People Power Party kimegawanyika kuhusu mgogoro huo, lakini kimesema kitaipinga kura hiyo.
Chama cha Democratic kinahitaji angalau wabunge wanane kati ya 108 wa chama tawala kuunga mkono hoja hiyo ili ipitishwe na theluthi mbili ya wingi wa kura za bunge hilo lenye viti 300.