1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa upinzani wavuruga kikao Albania

1 Oktoba 2024

Wabunge wa kambi ya upinzani nchini Albania wamekivuruga kikao cha bunge kupinga hatua ya kufungwa jela mbunge mwenzao kwa tuhuma za kusema uwongo.

Albanien, Tirana
Maafisa usalama wakizima moto baada ya wabunge wa upinzani kufanya vurugu bungeni nchini Albania.Picha: Florion Goga/REUTERS

Wabunge hao walisema kufungwa kwa Ervin Salianji ni hatua iliyochochewa kisiasa na wameitisha maandamano makubwa ya kuufunga mji mkuu, Tirana, kuanzia wiki ijayo.

Kwa miaka kadhaa sasa, chama cha upinzani cha kihafidhina cha Democratic nchini Albania kimekuwa kikitoa tuhuma kwamba chama tawala cha Kisoshalisti kimeyanyakua kwa nguvu madaraka yote, yakiwemo ya mahakama.

Soma zaidi: Albania yaidhinisha mkataba wa kuwahifadhi wahamiaji

Chama hicho cha upinzani kimekuwa kikiendesha maandamano ya vurugu ya kuipinga serikali tangu mwaka 2013.

Katika tukio la Jumatatu (Septemba 30), wabunge wa chama hicho walimshambulia spika pamoja na mawaziri wa serikali kwa kuwarushia vitu pamoja na kuvitia moto viti.