Wabunge waitisha amani mashariki ya Kongo
1 Machi 2023Wakati huu ambapo bado mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo yakiendelea katika baadhi ya maeneo wilayani masisi, wabunge waliochaguliwa mkoani kivu kaskazini, wamemtaka rais wa nchi hiyo kugeukia njia ya mazungumzo ya amani badala ya vita vinavyo endelea kuyagharimu maisha ya wananchi mkoani humo
Katika tangazo lao jana Jumatatu, wabunge hao kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa hapa nchini Kongo, wamesema wamegadhabishwa na vita hivi vinavyo endelea kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 wanaosonga mbele kwa kasi kuviteka vijiji mkoani kivu kaskazini.
Soma pia:Mapigano baina ya jeshi la DRC na waasi wa M23 yazuka licha ya miito ya kusitisha vita
Hata hivyo, wabunge hao walio ingia likizoni tangu kuwekwa kwa utawala wakijeshi katika mikoa ya kivu kaskazini na ituri miaka miwili hivi sasa, wamehitaji njia zakidiplomasia badala ya vita hivi ambavyo wamesema vinawalazimisha maelfu kukimbia
Hili limekuwa ni tangazo la kwanza la wabunge hao wa kuchaguliwa tangu kuzuka kwa mapigano hayo ambayo kinshasa imekuwa ikiituhumu Rwanda kulisaidia kundi hilo la M23 madai ambayo yameendelea kukanushwa na serikali ya kigali. Hata hivyo, mawakala wa sasi za kiraia wamewatuhumu wabunge hao kula kula njama na makundi ya waasi na kukwamisha juhudi zakutafuta amani maeneo hayo
Hadi sasa, waasi wa 23 wameaudhibiti mji mdogo wa Mweso takribani kilometa 100 kaskazini mwa mji wa Goma baada yakuchukua udhibiti wa Mushaki nakukalia kwa muda mji wa madini wa Rubaya wilayani masisi ambamo walitimuliwa na wapiganaji wakizalendo.
Aidha, licha ya ratiba iliyo chapishwa na viongozi wakikanda Februari 17 iliyoyataka makundi yenye silaha kuanza kuondoka kwenye maeneo yanayo shikilia kuanzia februari 28, waasi hao wa M23 wanasonga mbele huko masisi nakusalia katika ngome zao mbalimbali wilayani Rutshuru na nyiragongo.
Benjamin Kasembe/DW-Goma