Wachezaji wa Bayern warejea kutoka likizo fupi ya Ibiza
13 Mei 2025
Thomas Müller, Harry Kane na mlindalango Manuel Neuer walikuwa miongoni mwa wachezaji ambao kwa mujibu wa gazeti la Bild walikuwa wamefanikiwa kufanya safari hiyo ya likizo siku iliyotangulia.
Ziara hiyo ilikuwa imekosolewa kwa sababu msimu haujakamilika bado na wapinzani wa mwisho wa Bayern, klabu ya Hoffenheim hawako salama kikamilifu kutokana na uwezekano wa kukabiliwa na shoka la kushuka daraja.
Hoffenheim wako alama tatu mbele ya Heidenheim katika nafasi ya kucheza mechi za mchujo na wana tofauti kubwa ya mabao sita ya kufunga na kufungwa.
Kocha wa Bayern Vincent Kompany alikuwa amewapa wachezaji wa kikosi chake siku chache za mapumziko baada ya kubeba taji la Bundesliga Jumamosi iliyopita.
Wachezaji wa Bayern walikuwa tayari wamepanga safari ya kwenda Ibiza wiki iliyotangulia baada ya kushinda taji la Bundesliga lakini ikazuiwa kupitia kura ya turufu na viongozi wa klabu kwa sababu msimu ulikuwa bado haujakamilika.