1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachina katika miji kadhaa ya nchi hiyo waandamana kupinga uhuru wa Tibet

20 Aprili 2008

Beijing:

Maandamano ya kupinga uhuru wa jimbo la Tibet yameendelea katika miji kadhaa ya China leo ikiwa ni siku ya pili. Waandamanaji walikusanyika katika duka kubwa la kifaransa mjini Beijing "Carefour" wakipiga kelele kuiunga mkono Jamhuri ya umma wa China na kupinga uhuru wa Tibet.Duka hilo limelengwa kutokana na madai kwamba kampuni ya Carefour ina mafungamano na watibeti wanaoishi uhamishoni, huku kukitolewa wito wa kuzisusia bidhaa zinazotoka Ufaransa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW