Wachina waandamana Burundi
22 Novemba 2007Matangazo
BUJUMBURA:
Wafanyabiashara wa Kichina wameandamana mitaani katika mji mkuu wa Burundi,Bujumbura wakitaka usalama zaidi,baada ya mmoja wao kuuawa juma lililopita.Kiasi ya waandamanaji 30 walisimama mbele ya ofisi ya rais na wizara za sheria na masuala ya nje na wakawasilisha barua ya malalamiko yao.
Juma lililopita,watu wenye bunduki walimuua Wu Shengfang katika kiwanda chake cha ngozi kabla ya kutoroka kwa pikipiki.Majambazi hao bado hawajakamatwa.Nchini Burundi,kuna kiasi ya Wachina 100 na kama theluthi moja yao ni wafanyabiashara.