1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Wachunguzi Korea Kusini waapa kumkamata Yoon

1 Januari 2025

Wachunguzi nchini Korea Kusini wamesema kuwa wataitekeleza hati ya kumkamata Rais Yoon Suk Yeol kabla ya muda wa mwisho wa Januari 6. Amejifungia nyumbani kwake kwa wiki kadhaa akikwepa juhudi za kutaka kumhoji.

Rais Yoon Suk-yeol akilihutubia taifa baada ya kuifuta amri ya kijeshi
Rais Yoon amejifungia nyumbani kwake kwa wiki kadhaa akikwepa juhudi za wachunguzi za kutaka kumhojiPicha: South Korean Presidential Office/Getty Images

Wafuasi na wapinzani wa Yoon, aliyeachishwa kazi kupitia kura ya bunge kuhusu jaribio lake la kuondoa utawala wa kiraia mwezi uliopita, wamekita kambi nje ya makazi yake. Amejifungia nyumbani kwake kwa wiki kadhaa akikwepa juhudi za wachunguzi za kutaka kumhoji.

Mkuu wa Ofisi ya Uchunguzi wa Rushwa Dong-woon amewaambia waandishi habari kuwa wanalengakutekeleza agizo la kumkamata rais hiyo bila usumbufu, lakini pia wanashirikiana na polisi na maafisa wengine katika maandalizi. Aidha ameonya kuwa yeyote anayejaribu kuwazuia maafisa kumkamata Yoon atashitakiwa.

Amesema wanavichukulia vitendo kama vile kuweka vizuizi ili kupinga utekelezaji wa waranti wa kumkamata rais huyo kuwa ni kizingiti cha uendeshwaji majukumu rasmi. Haijafahamika kama watafaulu kuitekeleza waranti hiyo ya kumkamata kwa sababu Idara ya Ulinzi wa Rais hapo awali ilikataa kuheshimu hati za kufanywa upekuzi nyumbani kwake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW