Wadau wa ustawi wa chakula wa Afrika wakutana Dar es Salaam.
5 Septemba 2023Kongamano hilo la siku tatu linalomulikaa na kuchambua ni kwa kiasi gani nchi za Afrika zinavyoweza kujinasua katika baa la ukosefu wa chakula cha uhakika hasa wakati huu ambako dunia imetoa katika kitisho cha janga la virusi vya corona na vita vya Urusi na Ukraine vinavyoendelea.
Washiriki wanatilia mkazo majadiliano yanayolenga mabadiliko ya mifumo ya chakula na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuwa na uhakika wa chakula kwa wote.
Mikakati ya Tanzania katika kustawisha kilimo.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dr Philip Mpango aliyezindua kongamano hilo linalowaleta pamoja zaidi ya washiriki 3,000 alitaja mikakati inayochukuliwa na serikali ya Tanzania katika kuleta mapinduzi ya kijani ya kilimo.
Uanzishwaji wa miradi inayowalenga vijana na wanawake, kuongezwa kwa bajeti ya kilimo pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa, ni baadhi ya mambo aliyoyataja akisema mambo kama hayo yanapaswa kutiliwa mkazo pia nan chi nyingine barani humu ili kufiikia ajenda ya pamoja ya afrika ya mwaka 2030.
Hata hivyo, alilaumu kuhusu mizozo na vita inayoshuhudiwa katika sehemu nyingi za Afrika yamesababisha wananchi wengi kuwa mateka wa chakula.
Uhakika wa chakula bado changamoto.
Usalama na ukosefu wa chakula cha uhakika bado ni suala tete linaloendelea kugonga vichwa vya wengi na kwamba nchi nyingi za Afrika ndizo zinazojikongoja zaidi. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa, katika watu watano, mmoja kati yao analala nja kila siku kutokana na kukosa chakula.
Baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wanasema kufanyika kwa makongamano kama hayo, ni hatua mojawapo ya kuzisaidia nchi za afrika kuvuka katika kizingiti hicho.
Jackson Mathius wa chama cha wataalamu wa lishe nchini Tanzania anaona sema mbali ya wataalamu na watunga sera kukutana katika makongamano ya namna hiyo, lakini mataifa yanapaswa kuongeza juhudi katika uzalishaji wa mazao ya kilimo
Soma zaidi:Wadau wajadili kilimo cha kulinda mazingira mjini Kampala
Kongamano hilo la siku tatu litahitimishwa kwa kuwekwa malengo ya uboreshaji mifumo ya chakula katika siku za usoni. Ama, Tanzania imelenga kutumia kongamano hilo kuonesha mafanikio yake katika sekta ya kilimo na kuwavutia wawekezaji wa ndani na kimataifa.
Chanzo: DW Dar es Salaam