1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wadau wajadili uhuru wa vyombo vya habari Tanzania

Tatu Yahaya3 Mei 2023

Dunia leo inaadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari, nchini Tanzania bado changamoto kadhaa zinashuhudiwa ikiwemo sheria zinazosimamia tasnia hizo kutajwa kupora uhuru wa vyombo vya habari

Weltspiegel 18.03.2021 | Tansania Kariakoo | Presse, Tod John Magufuli
Picha: AFP/Getty Images

Katika mbalimbali wamejikita katika kuangalia muskabali wa uhuru wa vyombo vya habari, katika taifa hilo la afrika mashariki ambalo lilishuhudia sheria zilizotungwa zikitumiwa kuminya uhuru wa habari, katika namna iliyotafsiriwa kuwa na nia ya kulinda maslahi mapana ya watawala.

Soma pia: Dunia yaadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari

Professor Chris Peter Maina anazitamaza sheria namna zinavyokinzana kati ya Tanzania bara na Zanzibar akisema sheria zinazotungwa katika bunge la Jamuhuri ya muungano wa tanzania zinalenga kutumika pande mbili za nchi lakini zile zinazotungwa na baraza la wawakilishi zanzibar hazitumiki kwa tanzania bara hivyo ametaka kuwa na sauti moja ya sheria itakayotambulika na kutumika kwa pande zote

Hali ya uhuru wa vyombo vya habari ikoje nchini mwako?

02:53

This browser does not support the video element.

Waandishi wa habari waliopo kazini wanataja ukinzani kati ya sheria hizo kuwa miongoni mwa changamoto kubwa linapokuja swala la kutekeleza majukumu yao ya kila siku wakitolea mfano baadhi ya mambo yanayokubalika upande wa bara lakini yasiokubalika kwa zanzibar hatua ambayo inawanyima uhuru katika kutekeleza majukumu yao na kutoa wito wakuwepo kwa sheria moja itakayo rahisisha kazi zao za kila siku. 

Soma pia: Maoni: Hali ngumu kwa vyombo vya habari Tanzania

Kando na hilo katika mjanda huo wa kitaifa ambao unaendelea baadae leo hii hoja ya kutengwa kwa watu wenye ulemavu linapokuja swala la haki habari linatawala kwa hadhira hiyo hasa viziwi na wasioona vyombo vya habari kama magezi kutozingatia nukta nundu huku program za televisheni zikishindwa kuzingatia viziwi isipokua taarifa za habari pekee.

Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa anasema sheria zipo zinazowabana wamiliki wa vyombo vya habari katika kulinda haki habari kwa makundi yote hivyo serikali inazingatia hilo na kuvitaka vyombo vya habari kuzingatia pia.

Kauli mbiu ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari inasema uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki nyingine za binadamu. Kongamano hili la vyombo vya habari limeandaliwa na wadau wa sekta ya habari, kikiwemo chuo cha mafunzo ya habari cha shirika la Utangazaji la Deutsche Welle, DW Akademie.