Wadephul akiri "hali tete" kwenye NATO chini ya Trump
13 Februari 2026
Akizungumza na kituo cha utangazaji cha Ujerumani, ARD mapema leo, Wadephul amekiri mivutano iliyoshuhudiwa katika siku za karibuni inaufanya ushirika huo wa kijeshi kuwa chini ya shinikizo kubwa.
Uhusiano baina ya Marekani na washirika wa NATO yameingia dosari tangu Rais Donald Trump aliporejea madarakani mwaka uliopita.
Trump pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi wa serikali yake wamekuwa wakiwakosoa vikali washirika wao wa Ulaya kwa kile ambacho Washington imesema ni kushindwa kuchangia vya kutosha kwenye bajeti ya ulinzi na kulitegemea zaidi jeshi la Marekani.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio anaiwakilisha nchi yake kwenye mkutano huo, unaohudhuriwa pia na viongozi wa Ulaya na Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen.