Wadephul aunga mkono sera ya umoja ya EU
4 Aprili 2026
Matangazo
Wadephul amesema haya katika mahojiano na shirika la habari la Funke yaliochapishwa leo Jumamosi.
Wadephul alitaja hasa mvutano na Hungary kuhusu mkopo mkubwa kwa Ukraine unaoungwa mkono na wanachama wengine wa Umoja huo wa Ulaya lakini kupingwa na Hungary. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Viktor Orbán ameishutumu Ukraine kwa kuzuia usambazaji wa mafuta ya Urusi hadi Hungary na Slovakia kupitia bomba la Druzhba, ambalo mwezi Januari, liliharibiwa na hatua ya kijeshi za Urusi huko Brody magharibi mwa Ukraine.
Wadephul amesema wanapaswa kufutilia mbali kanuni hiyo ya umoja katika sera za mambo ya nje na usalama kabla ya mwisho wa kipindi cha sasa cha bunge ili kuwezesha kuhudumu bora zaidi kimataifa na kwa uthabiti.