1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiArgentina

Rais wa zamani wa Argentina ashutumiwa kwa unyanyasaji

15 Agosti 2024

Ofisi ya mwendesha mashitaka nchini Argentina imemfungulia rasmi mashitaka Rais wa zamani Alberto Fernandez ya kumjeruhi vibaya aliyekuwa mkewe Fabiola Yanez.

Alberto Fernandez na Fabiola Yanez
Alberto Fernandez na Fabiola Yanez wakitembea kwenye zulia jekundu wakati huo Fernandez akiwa rais wa Argentina. Yanez hivi sasa anamshutumu Fernandez kwa kumnyanyasa kijinsiaPicha: CHANDAN KHANNA/AFP

Fabiola Yanez, ambaye kwa sasa anaishi Uhispania pamoja na watoto wake, wiki iliyopita alifungua kesi akimtuhumu Fernandez kwamba alimnyanyasa kijinsia kwa kumpiga wakati akiwa mkewe.

Picha zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari vilionyesha makovu kwenye mwili wa Yanez.

Wawili hao waliachana baada ya Fernandez kuondoka madarakani mwaka 2023.

Fernandez hata hivyo amesema shutuma dhidi yake ni za uwongo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW