1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamlaka zaifanyia upekuzi Deutsche Bank Ujerumani

28 Januari 2026

Benki mashuhuri ya Ujerumani Deutsche Bank imesema waendesha mashtaka wamefanya upekuzi katika baadhi ya ofisi zake kutokana na tuhuma za utakatishaji fedha.

Makao makuu ya Deutsche Bank, Frankfurt Ujerumani.
Benki mashuhuri ya Ujerumani Deutschen Bank inakabiliwa na tuhuma za kutakatisha fedhaPicha: Boris Roessler/dpa/picture alliance

Msemaji wa Deutche Bank amethibitisha Jumatano kuwa upekzi huo unafanyika katika ofisi hizo na kuwa inatoa ushirikiano kamili kwa waendesha mashtaka.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Süddeutsche, ukaguzi huo unahusiana na uvunjaji wa sheria katika biashara zinazofanywa kati ya benki hiyo na makampuni yanayohusishwa na bilionea wa Urusi Roman Abramovich.

Vita vya Ukraine vyatajwa

Mfanyabiashara huyo mkubwa aliwekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukrane. Gazeti hilo limesema ofisi zilizopekuliwa ni za Berlin na katika makao makuu ya benki hiyo mjini Frankfurt.  

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW