Waethiopia waandamana kulishangilia bwawa la umeme
3 Agosti 2020Matangazo
Bwawa hilo kubwa la umeme limejengwa kwenye mto Nile. Hata hivyo limeendelea kusababisha mvutano wa kikanda.
Maandamano hayo yaliitishwa kupitia mitandao ya kijamii, yumkini kwa kuungwa mkono na serikali.
Baadhi ya waandamanaji waliojawa na furaha walipiga miluzi, wengine walipiga honi za magari na muziki, huku wengine wakicheza dansi kwa kupeperusha bendera ya taifa pamoja na kuonyesha mabango yenye ujumbe unaohusiana na tukio hilo. Mikusanyiko kama hiyo ilifanyika pia katika miji mingine ya Ethiopia.
Naibu waziri mkuu wa nchi hiyo Demeke Mekonnen amesema shamra shamra hizo ni kusherehekea kuwanza kwa hatua ya mwisho katika ujenzi wa bwawa, ambalo amesema litaleta suluhisho la mwisho kwa matatizo mengi yanayoikumba Ethiopia.