1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAFA: Wapalestina 13 wameuawa kwa mashambulizi ya Israel

7 Septemba 2024

Wapalestina wasiopungua 13 wameuawa na wengine 15 wamejeruhiwa leo kwenye mashambulizi yaliyofanywa na ndege za Israel yaliyoilenga shule moja iliyokuwa ikiwahifadhi wakimbizi kwenye Ukanda wa Gaza.

Hali kwenye Ukanda wa Gaza
Hali kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Ramadan Abed/REUTERS

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la Kipalestina, WAFA. Watu 8 waliuawa kwenye mahema ya wakimbizi katika shule ya Al-Sa´diyya inayopatikana katika kitongoji cha Jabalia kaskazini mwa Gaza.

Wengine watano wameuawa pale Israel imepolilenga jumba moja la makaazi ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nuserat. Jeshi la Israel limesema shambulio dhidi ya shule lilikuwa na lengo la kuisambaratisha kamandi ya kundi la Hamas.

Hadi sasa jumla ya Wapalestina 40,800 wameuawa na vikosi vya Israel tanguilipoanzisha mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza kujibu hujuma iliyofanywa na Hamas Oktoba 7 mwaka jana ambapo watu 1,200 waliuawa ndani ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW