Wafadhili Berlin waahidi dola bilioni 1.3 kwa ajili ya Sudan
16 Aprili 2026
Matangazo
Ujerumani kwa upande wake imeahidi kutoa yuro milioni 230. Ahadi hizo za ufadhili zimekuja wakati ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo vimeingia mwaka wake wa nne.
Katika ujumbe alioutoa kwa njia ya video, Katibu Mkuuwa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema "jinamizi la vita huko Sudan ni sharti lifike mwisho."
Washiriki wengi wa mkutano huo wametoa wito wa usitishwaji mapigano mara moja kwa ajili ya misaada ya kiutu kama hatua ya kwanza kuelekea mchakato mpana wa amani ya kudumu.
Mwenyeji wa mkutano huo alikuwa Ujerumani kwa ushirikiano na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.