1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafadhili waahidi mabilioni ya dola kwa Syria

Admin.WagnerD5 Februari 2016

Mataifa fadhili Alhamisi (04.02.2015) yameahidi kutowa msaada wa mabilioni ya dola kwa wananchi wa Syria katika mkutano wa kushughulikia mzozo mbaya kabisa wa kibinadaamu duniani

Mkutano wa wafadhili London .(04.02.2015)
Mkutano wa wafadhili London .(04.02.2015)Picha: Getty Images/D. Kitwood

Kansela Angela merkel wa Ujerumani amesema "Ndio maana serikali ya Ujerumani ingelipenda kuahidi msaada wa euro bilioni 1.1 kwa ajili ya mipango ya misaada ya binaadamu kwa Umoja wa Mataifa. Milioni 570 kwa ajili ya Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa kama mchango wa kujalizia asilimia 50 ya fedha zinazohitajika na shirika hilo na nataraji hatimae tutakuwa tunaweza kusema kwamba hakutokuwa kuwa na haja ya kuwa na wasi wasi juu ya mgao wa chakula."

Kansela Angela Merkel ameahidi masaada wakibinaadamu wa euro bilioni 2.3 kwa Syria kufikia mwaka 2018 ikiwa ni pamoja na euro bilioni 1.2 mwaka huu.

Wakati vita vya miaka mitano nchini Syria vikizidi kupamba moto na jaribio jengine la mazungumzo ya amani mjini Geneva likiahirishwa baada ya siku chache tu, mkutano huo wa wafadhili mjini London unakusudia kushughulikia mahitaji ya takriban watu milioni sita waliopeteza makaazi yao ndani ya Syria kwenyewe na wengine zaidi ya milioni 4 wakimbizi walioko katika nchi nyengine.

Maelfu waelekea Uturuki

Akisisitiza hali ya kutapatapa ilioko nchini Syria Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu ameuambia mkutano huo kwamba makumi ya maelfu ya Wasyria wanakimbilia nchini mwake kuepuka mashambulizi ya mabomu katika mji wa Allepo.

Kansela Angela Merkel akizungumza katika mkutano wa wafadhili London (04.02.2015)Picha: Getty Images/D. Kitwood

Amesema watu sitini hadi sabini elfu walioko kwenye makambi kaskazini mwa Aleppo wanaelekea Uturuki na kwamba akili yake hivi sasa haiko London iko mpakani ambapo ameuliza vipi wanaweza kuwapangia makaazi wakimbizi hao wapya.

Uturuki tayari inawahifadhi zaidi wa wakimbizi milioni 2.5 wa Sryria.

Camroon aongezea sauti yake

Waziri Mkuu wa Uingereza ambaye nchi yake ndio mwenyeji wa mkutano huo David Cameroon alikuwa mmojawapo wa wazungumzaji ambapo amesema"Kama vile Angela Merkel alivyosema leo inapaswa kuwa siku ya matumaini ambapo hali ni ngumu sana katika mzozo wa Syria leo ni siku kuhusu ufadhili wa wakimbizi, kuwasaidia watu hao, kuzisaidia familia zao,kuwasomesha watoto wao kuwapa heshima ya kufaya kazi . Hii ndio inayoamanisha siku ya leo."

Wazungumzaji wengine kadhaa pia wamesema wakati hali ya wakimbizi ni mbaya ile ya Waysria waliokwama ndani ya nchi hiyo na kukabiliwa na mashambulizi ya mabomu, kuzingirwa na katika baadhi ya sehemu kufa njaa haisemeki.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaomba dola bilioni 7.73 kukabiliana na hali ya dharura nchini Syria mwaka huu.Uingereza,Norway na Ujerumani ni nchi za mwanzo kutangaza misaada yao zikifuatiwa na Marekani, Umoja wa Ulaya na Japani.

Mwandishi : Mohamed Dahman/Reuters

Mhariri :Gakuba Daniel

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW