1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Wafadhili wakutana Paris kusaidia Ukraine

13 Desemba 2022

Mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa yanakutana mjini Paris Ufaransa katika juhudi mpya za kuchanga fedha kusaidia Ukraine irejeshe miundo mbinu yake ya nishati, na ipate chakula.

Frankreich, Paris |  Ukraine Konferenz
Picha: Teresa Suarez/POOL/AFP/Getty Images

Mashambulizi yanayoendelea ya Urusi dhidi ya nchi hiyo yamewatumbukiza mamilioni ya watu kwenye baridi na giza msimu huu wa baridi.

Mkutano huo wa kimataifa wa wafadhili unatarajiwa kuchangisha mamilioni ya dola kwa misaada.

Mkutano huo unalenga zaidi kusaidia Ukraine kushughulikia mahitaji ya maji, nishati, chakula, afya na uchukuzi hadi mwisho wa mwezi Machi.

Waandaaji wamesema unalenga pia kutuma ujumbe kwa serikali ya Urusi kwamba jamii ya kimataifa inasimama na Ukraine dhidi ya mashambulizi yake ambayo yameharibu sekta ya nishati na miundombinu muhimu ya Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW