1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanya kazi 26 wauawa katika migodi ya Uchina:

27 Desemba 2003
BEIJING: Wafanya kazi 26 wameuawa ulipotokea moto katika mgodi wa makaa katika jimbo la Uchina ya Kaskazini, Hebei. Shirika la Habari la Uchina, XINHUA, limeripoti kuwa moto huo ulisababishwa na mripuko wa waya za umeme. Wafanya kazi kumi wameweza kujinusuru wenyewe. Maafa hayo yalitokea katika mgodi wa makaa mjini Wuan. Mara kwa mara hutokea ajali kama hizo katika migodi hiyo iliyo mikukuu mno huko Uchina ya Kaskazini. Watu wapatao 7,200 wameuawa peke yake katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu ilisema taarifa ya serikali.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW