Wafanyakazi Italia wagoma kuonyesha mshikamano na Gaza
23 Septemba 2025
Maelfu ya waandamanaji na wafanya migomo wanaoshinikiza mshikamano na raia wa Kipalestina huko Gaza, walimiminika mitaani nchini Italia jana, huku baadhi wakivamia kituo kikuu cha treni mjini Milan na kukabiliana na polisi. Vyama vya mashinani nchini Italia, ambavyo vinawakilisha mamia kwa maelfu ya watu kuanzia walimu wa shule hadi mafundi vyuma, vilitoa wito wa kufanyika kwa mgomo wa saa 24 katika sekta za umma na binafsi, zikiwemo usafiri wa umma, treni, shule na bandari. Mgomo huo umetatiza shughuli kadhaa kote nchini humo ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa treni za masafa marefu na usafiri wa umma katika miji mikubwa ikiwemo Roma. Zaidi ya watu 20,000 walikusanyika mbele ya kituo kikuu cha Roma kulalamikia hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea Gaza.