1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa UN washikiliwa na Waasi wakihouthi Yemen

7 Juni 2024

Takriban wafanyakazi 9 wa mashirika ya Umoja wa Mataifa,raia wa Yemen wamekamatwa na wanashikiliwa na waasi wa Houthi chini ya mazingira yasiyoeleweka ndani ya taifa hilo.

Jemen Sanaa | Wapiganaji wa Kihouth
Wapiganaji wa Kihouth wakiwa katika oparesheni.Picha: Yahya Arhab/EPA

Hayo yameleezwa leo na mamlaka za Yemen katika wakati ambapo waasi hao wanakabiliwa na shinikizo la kiuchumi linaloongezeka pamoja na mashambulizi ya anga ya  muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani.  

Maafisa wa kikanda ambao hawakutaja majina kwasababu hawana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo,wamelithibitishia shirika la habari la Associated Press juu ya tukio la kuzuiliwa kwa wafanyakazi hao wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo WFP,na shirika la haki za binadamu.

Soma pia:Waasi wa Kihuthi waapa kujibu mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umekataa kutowa tamko lolote kuhusu kadhia hiyo. Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wamekuwa wakizilenga meli zinazopita katika bahari ya Sham kufuatia vita vya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.