Abay Kassahun amejitolea kuwasaidia wanawake walio nyanyaswa nchi za nje walipokuwa wakitafuta maisha bora. Mbali na msaada wa kisaikolojia, wengine wanahitaji matibabu na ushauri wa daktari. Huwa anwatembelea wagonjwa wake hata majumbani mwao. Kazi zimempelekea kupata jina la utani: muuguzi wa kusafiri.