SiasaUingereza
Wafanyakazi wa idara ya uhamiaji Uingereza waanza mgomo
3 Aprili 2023Matangazo
Mgomo huo ndio hatua ya karibuni kabisa kuchukuliwa katika nchi hiyo iliyoandamwa na migomo kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha ambayo haijawahi kuonekana kwa miaka mingi.
Chama cha wafanyakazi wa idara ya umma na biashara PCS kimeishutumu serikali kwa kushindwa kuwashughulikia wafanyakazi wa sekta ya umma.
Wanataka yafanyike mazungumzo kuhusu mishahara, ajira, pensheni na mazingira ya kazi. Vyama vya wafanyakazi vinasema wanachama wao wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha kutokana na mfumko wa bei na kutopanda kwa viwango vya mishahara.
Zaidi ya wafanyakazi 1000 wa idara inayoshughulikia masuala ya hati ya usafiri wanajiandaa kushiriki mgomo huo. Aidha mgomo wa nchi nzima wa sekta ya umma umepangwa kufanyika tarehe 28 Aprili.