1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa misaada wapatikana wiki moja baada ya kutekwa

5 Mei 2023

Wafanyakazi wawili kati ya watatu wa shirika la misaada waliotekwa nyara kaskazini mashariki mwa Nigeria wamekutwa salama, wiki moja baada ya kutekwa.

Nigerianischer Soldat
Picha: FLORIAN PLAUCHEUR/AFP

Wafanyakazi hao wa Kinigeria wanafanya kazi katika shirika linalotoa huduma za kibinaadamu la Marekani, FHI 360, na walitekwa nyara Aprili 25 kutoka Ngala, kwenye jimbo la Borno karibu na mpaka wa Cameroon.

Msemaji wa shirika hilo, Christy Delafield, amesema wamearifiwa kwamba polisi wa Nigeria wamewapata wafanyakazi wake wawili.

Hata hivyo, Delafield hajaeleza iwapo wafanyakazi hao waliokolewa au walifanikiwa kutoroka.

Soma zaidi: Ufanisi mdogo katika ushirikiano kati ya Boko Haram na IS

Wakandarasi wawili pia walitekwa nyara na bado hawajulikani walipo, pamoja na mfanyakazi wa tatu wa shirika hilo la misaada.

Vyanzo viwili vya usalama, ambavyo havikutaka kutajwa jina, vimesema kwamba wafanyakazi hao waliokolewa kutoka kwenye kambi ya wapiganaji wanaofungamana na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, kanda ya Afrika Magharibi ( ISWAP) katika kijiji cha Gargash siku ya Jumapili.