1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa ndani Lebanon wako mashakani - UM

4 Oktoba 2024

Umoja wa Mataifa unasema wafanyakazi wa majumbani nchini Lebanon, wengi kutoka mataifa ya Afrika na Asia, wanapitia kipindi kigumu, ikiwemo kutelekezwa na waajiri wao wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea.

Lebanon | Israel Beirut
Matokeo ya mashambulizi ya Israel kwenye makaazi ya watu mjini Beirut.Picha: Hassan Ammar/AP Photo/picture alliance

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Uhamiaji la Umoja huo (IOM) imesema baadhi ya wafanyakazi wa ndani wamefungiwa majumbani wakati waajiri wao wakikimbia mashambulizi ya anga ya Israel.

 Wengine wametelekezwa mitaani bila ya kuwa na maeneo ya kujihifadhi.

Soma zaidi: Iran yaahidi kuishambulia tena Israel endapo itashambuliwa

IOM imefichuwa madhila wanayopitia zaidi ya wafanyakazi wa kigeni 170,000 waliopo nchini Lebanon, wengi wao wakiwa wanawake kutoka mataifa kama Ethiopia, Kenya, Sudan, Sri Lanka, Bangladesh na Ufilipino. 

Shirika hilo limesema hivi sasa linapokea maombi mengi kutoka kwa wahamiaji hao ya kutaka kusaidiwa kurejea makwao. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW