1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wahamiaji Israel wakabiliwa na hali ngumu

Angela Mdungu
27 Oktoba 2023

Zaidi ya wiki mbili sasa tangu Israel ilipojibu mapigo ya kundi la Hamas kwa kuilipua Gaza kupitia mashambulizi ya ndege na imeapa kulisambaratisha kundi la Hamas la Palestina

Miji ya Gaza iliosahambuliwa na Israel
Miji ya Gaza iliosahambuliwa na IsraelPicha: Mohammed Dahman/AP/picture alliance

Wakati wahamiaji wanaofanya kazi nchini humo na ndugu zao kwenye mataifa wanakotoka wakihofia usalama wa wahamiaji hao, baadhi wanasema, hawako tayari kuacha kazi zao Israel.

Wiki iliyopita, Waziri wa mambo ya kigeni wa Thailand aliratibu kurejeshwa nyumbani kwa raia wake ambao ni wahamiaji waishio Israel.

Ufilipino nayo ilisemaitatoa misaada ya kifedha na dawa kwa wahamiaji wa taifa hilo waishio nchini humo na kuwa itagharamia kurejeshwa kwao nyumbani.

Soma pia:Israel imesema inajiandaa na mashambulizi ya ardhini ikilenga kuliangamiza kundi la wanamgambo wa Hamas

Thailand na Ufilipino ndizo zenye idadi kubwa ya wafanyakazi wa kigeni Israel ambapo kila moja ina watu wasiopungua 30,000.

Mauaji ya wafanyakazi wahamiaji nchini humo yamesababisha mshtuko kwa takribani wafanyakazi 110,000 wa kigeni ambao wanaishi kihalali Israel hali ambayo imepelekea wengi wao kujipanga kuondoka. 

Wafanyakazi wahamiaji watekwa na kuuwawa

Kulingana na serikali ya Thailand, watu wake karibu 30 wengi wao wakiwa wakulima waliuwawa , 16 walijeruhiwa na 17 ni kati ya waliochukuliwa mateka wakati Hamas iliposhambulia miji ya Israel na kuwauwa watu wasiopungua 1,400 mapema mwezi huu. 

Mtalii akiwa na mizigo yake akiondoka IsraelPicha: Oliver Weiken/dpa/picture alliance

Soma pia:Israel yafanya shambulio jingine Ukanda wa Gaza

Kamlue, mkulima raia wa Thailand mwenye miaka 41 aishiye Israel ambaye hakutaka kutajwa jina kamili anasema alikuwa akielekea kwenye mavuno karibu na mpaka wa Gaza Oktoba 7 wakati lori alimokuwemo lilipoanza kushambuliwa.

Anaeleza kuwa wavamizi hao walimimina risasikutoka pande zote. Dereva wa lori hilo alifanikiwa kulifikisha sehemu salama lakini Kamlue ni mmoja wa waliojeruhiwa. Alipigwa risasi mguuni na bado anaendelea kupata ahueni.

Licha ya masaibu hayo, Kamlue ambaye alirejea nyumbani kupitia ndege maalumu ya serikali ya Thailand bado anapanga kurejea Israel kufanya kazi ili aweze kulipa madeni yake mara tu hali ya usalama itakapoimarika.

Kwa upande wake, Marivic Yape, mfanyakazi  wa  kifilipino aliyewasili Israel Juni 2022 aliiambia taasisi ya Thomson Reuters kuwa hana budi kuendelea kufanya kazi nchini humo ili alipe deni la dola za kimarekani 3,527.

Soma pia:UN yasema msaada usio na kikomo unahitajika Gaza

Ingawa sekta ya utalii kwa sasa imezorota, Yape anasema alikuwa akifanya kazi muda wote tangu vita vilipoibuka.

Israel kuuzingira Ukanda wa Gaza

02:48

This browser does not support the video element.

Anasafisha vyumba kwenye hoteli zilizokuwa zikiwahifadhi Waisraeli waliohamishwa kutoka kwenye jamii zinazoishi karibu na ukanda wa Gaza.

Yape anabainisha kuwa walisafisha vyumba kuliko awali ingawa walikuwa na hofu.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka katika mji wa Eilat amesema watu pekee waliokuwa wakionekana nyakati za usiku ni wafanyakazi wa aina yake.

Singh Donfueng 38, mfanyakazi raia wa Thailand katika mashamba, aliwasili mwezi Mei.

Ameeleza kuwa anapanga kuendelea kukaa Israel ili alipe deni la dola 2,766 ingawa ndugu zake wanahofia usalama wake na wanataka arejee nyumbani.

Wengi waomba ushari kwa mashirika ya wahamiaji

Msemaji wa Shirika la hisani la haki za wahamiaji la Israeli liitwalo  Kav LaOved, Assia Ladizhinskaya amesema shirika hilo limekuwa likipokea simu nyingi kutoka kwa wahamiaji wanaoomba ushauri kuhusu mahali pa kwenda ili wabaki salama.

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiandaa misaada kwa ajili ya GazaPicha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Mbali na kuhofia usalama pia, haki zao na ikiwa wanaweza kupata misaada kutoka serikalini kama hakutakuwa na kazi- Katika baadhi ya sehemu za nchi zinazolengwa na mashambulizi ya roketi ya wapiganaji wa Hamas wa Gaza au kundi la Hezbollah la Lebanon, kufungwa kwa shughuli za uchumi kumesababisha wahamiaji wengi kubaki bila kazi.

Soma pia:Miito imekuwa ikongezeka ya kufunguliwa kwa njia salama na zisizo na vizuizi za kupitisha misaada ya kiutu hadi Gaza
 
Makundi ya haki za wafanyakazi yamesema vita kati ya Israel na kundi la Hamas vimeonesha baadhi ya matatizo yanayowakabili wafanyakazi wa kigeni katika maeneo yenye mizozo.

Kuhusu masaibu hayo serikali ya Israel iliandika barua kwa njia ya mtandao kwa wahamiaji.

Barua hiyo imeeleza kuwaimeongezea muda wa vituovya huduma kwa wateja kwa wafanyakazi wa kigeni na kwamba imetoa maelekezo ya hatua za kiusalama kwa lugha mbalimbali.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW