1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafaransa wapiga kura duru ya pili ya uchaguzi wa Bunge

7 Julai 2024

Raia wa Ufaransa wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa bunge ambao yumkini utakipatia ushindi wa kihistoria chama cha mrengo mkali wa kulia cha National Rally (RN).

Marine Le Pen
Kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha National Rally (RN) Marine Le Pen Picha: Jonathan Rebboah/Panoramic/IMAGO

Chama hicho kinachoongozwa bungeni na mwanasiasa Marine Le Pen kinapendelea sera za kizalendo na kuyaweka mbele maslahi ya Ufaransa kwanza na vilevile kinapinga suala la uhamiaji.

Uchaguzi huu wa bunge utaamua iwapo RN itanyakua majimbo mengi au Ufaransa itapata bunge ambalo hakuna chama chenye udhibiti kamili.

Uchaguzi huo utakuwa na taathira siyo ndani ya Ufaransa pekee bali pia kimataifa. Mathalani utaamua kuhusu hatma ya msaada ambao Ufaransa inautoa kwa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi na uthabiti wa kiuchumi kwenye kanda ya Umoja wa Ulaya. 

Kambi ya rais Macron yatwaa ushindi uchaguzi wa bunge

Ufaransa imo kwenye ukingo wa kupata serikali ya kwanza ya mrengo mkali wa kulia tangu vikosi vya Manazi vya Ujerumani vilipoikamata na kuikalia nchi hiyo kwa mabavu wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Iwapo RN kitashinda wingi mkubwa wa vita bungeni kiongozi wake Jordan Bardella  atakuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW