Wafaransa wapiga kura kumchaguwa rais
23 Aprili 2017Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, Marine Le Pen, na wa siasa za wastani Emmanuel Macron wanatarajiwa kuongoza katika duru hiyo na kuingia katika duru ya pili itakayofanyika Mei 7, lakini mchuano ni mkali katika taifa hilo lililogawanyika kwa sasa. Waangalizi wanatabiri ushindi wa Le Pen unaweza kuwa pigo kwa Umoja wa Ulaya, ambao tayari umedhoofishwa na kura ya maoni ya Ungereza ya kujiondoa katika umoja huo.
Macron, mwenye umri wa miaka 39, anagombea kuwa rais wa kwanza wa Ufaransa mwenye umri mdogo, na amekuwa akiuunga mkono Umoja wa Ulaya pamoja na maendeleo ya kibiashara katika kampeni zake.
Upigaji kura umwekwenda kinyume na matabirio ya kujitokeza kwa idadi ndogo ya wapiga kura baada ya kampeni za uchaguzi kutawaliwa na kashfa na kushuka kwa umashuhuri wa vyama vikuu ambayo vimekuwa vikipokezana madaraka kwa nusu karne iliopita.
Idadi kubwa yajitokeza
Baada ya masaa tisa ya kupiga kura idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa asilimia 69.42 mojawapo ya kiwango cha juu kabisa kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 40.Kikiwa chini kidogo ya kiwango cha uchaguzi wa mwaka 2012, saa moja ya ziada ya kupiga kura katika miji midogo inatarajiwa kukifanya iwango hicho kufikia asilimia asilimia 78 hadi 81.
Le Pen amepiga kura yake huko Henin-Beaumont mji uliokuwa ukizalisha makaa ya mawe hapo zamani ambayo ni ngome ya chama chake kaskazini mwa nchi hiyo.
Macron amepiga kura katika mji wa kitalii wa Le Touquet akiwa pamoja na mke wake Brigitte mwalimu wake wa shule wa zamani ambaye ni mkubwa wake kwa miaka 25.Fillon na Melenchon wote wawili wamepiga kura zao mjini Paris.
Takariban watu milioni 47 wanastahiki kupia kura katika taifa hilo la kanda ya sarafu lenye kushika nafasi ya ili kwwa kuwa na guvu kubwa za kiuchumi.
Uchaguzi warindima nje ya mipaka.
Wakati wapiga kura wakipiga kura katika uchaguzi huo wanafanya chaguo ambalo litarindima kupindukia mipaka ya Ufaransa kuanzia medani za vita nchini Ufaransa sakafu za biashara huko Hong Kong na kumbi za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Mustakbali wa Ulaya uko hatarini wakati nchi hiyo ikikabiliwa na uchaguzi tafauti na nchi nyengine ambao yumkini ukarekebisha utambulisho wa Ufaransa wa baada ya kipindi cha vita na kuashiria iwapo sera kali za mrengo wa kulia zinaongezeka au kupunguwa.
Takriban wagombea wote 11 wefanya kampeni dhidi ya Umoja wa Ulaya ambao unalaumiwa kwa matatizo lukuki.Wagombea wawili kati ya hao wana nafasi ya kushinda uchaguzi huo wa rais mwanasiasa wa sera kali za mrengo wa kulia Marie Le Pen na yule wa sera kali za mrengo wa kushoto Jean- Luc wanaweza kutaka kujitowa kwa Ufransa katika umoja huo pamoja na matumizi yao ya pamoja ya sarafu ya euro.
Kujitowa kwa Ufaransa kutakuwa balaa
Kujitowa kwa Ufaransa katika umoja huo kutakuwa kubaya zaidi kuliko kule kujitowa kwa Uingereza kutaashiria kifo kwa Umoja wa Ulaya,sarafu ya euro na fikra nzima ya umoja wa Ulaya iliozaliwa kutokana na damu iliomwagika wakati wa Vita Vikuu vya Dunia.
Ufaransa ni taifa manachama muasisi wa Umoja wa Ulaya na inashikilia kiti cha udereva pamoja na mwanachama mwenzake Ujerumani.
Masoko ya fedha tayari yana wasi wasi juu ya uwezekano wa kujitowa kwa Ufaransa katika Umoja wa Ulaya Frexit yakihofia udhibiti wa kuhamisha fedha,kuondolewa kwa mtaji,kufilisika na kesi za madai juu ya hati za dhamana na kondarasi.Timu ya Le Pen haizipi uzito habari za kutokea maangamizi ya aina hiyo kwa hoja kwamba itakavyokuwa sarafu ya euro inaelekea kusambaratika.
Le Pen na Melenchon pia wanalaumu mikataba ya biashara huru kwa kuuwa ajira za Ufaransa na wanataka kuijadili upya jambo ambalo litasababisha mzongo wa kifedha kwa umoja wote wa Ulaya na washirika wa biashara wa Ufaransa.
Iwapo Le Pen au Melenchon wataingia duru ya pili huo utaonekana kuwa ushindi wa wazi kwa kwa wimbi la sera kali za mrengo wa kulia lililonyeshwa wakati wa kumchaguwa Rais Donald Trump wa Marekani na kujitowa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.
Marekebisho sheria za ajira
Emmamuel Macron wa sera za wastani na mhafidhina Francois Fillon wamejitolea kwa umoja wa Ulaya na watazifanyia mageuzi sheria za kazi lakini hawatofanya mabadiliko makubwa sana. Macron amejitangaza kama mgombea dhidi ya sera kuhami masoko za Trump.
Ufaransa ambayo ina nguvu za silaha za nyuklia na kiti katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ina maelfu ya wanajeshi wake duniani na ni mshirika wa karibu wa Marekani katika kampeni ya kupambana na kundi linalojiita Dola la Kiislam.
Macron yumkini akaendeleza operesheni dhidi ya wapinagaji wa itikadi kali nchini Iraq na Syria na kanda ya Sahel barani Afrika pamoja na kuishinikiza Urusi kuhusiana na suala la Ukraine na hatua zake za kumpa nguvu Rais Bashar al Assad wa Syria.
Mwandishi : Mohamed Dahman/AP
Mhariri : Yusra Buwayhid